CONSULTANT

MJENWA

  • mjengwa.blogspot.com

Wednesday, 10 February 2010

China inasema itaweka kodi kubwa dhidi ya bidhaa za Marekani zinazotokana na mifugo ambazo zinaingizwa China kwa wingi. Wizara ya biashara ilitangaza Ijumaa inaweka ushuru baada ya uchunguzi kubaini kuwa bidhaa za kuku zilikuwa zinauzwa kwa gharama ndogo isivyostahili, ambayo imeumiza wazalishaji wa ndani.

China inasema kodi hiyo itaanza Februari 13. Makampuni ambayo walikata rufaa kuhusu suala hilo ikiwemo kiwanda kimoja cha mifugo cha Marekani cha Tyson Foods, watalipa ushuru kati ya asilimia 43 na 80. Wale ambao hawakukata rufaa watalipa ushuru wa asilimia 105.4.

Ushuru huo upo kwenye bidhaa mbali mbali ikiwemo miguu ya kuku, ambayo sio maarufu sana kwa wanunuzi wa Marekani, lakini ni maarufu huko China. China na Marekani wamekuwa kwenye mlolongo wa mivutano ya kibiashara katika miaka ya karibuni.

China ilianzisha uchunguzi wake juu ya uingizaji kuku wa Marekani mwezi Septemba, baada ya utawala wa Obama kuongeza kodi ya matairi yanayotengenezwa nchini China. Beijing pia imekasirishwa na mkataba wa karibuni wa silaha unaogharimu dola bilioni 6.4, kati ya Washington na Taiwan, kisiwa kinachojitawala ambapo China inakiona kama sehemu ya eneo lake na azma ya Rais wa Marekani Barack Obama kufanya mazungumzo na Dalai Lama, kiongozi wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni.




E-mail Chapisha

No comments:

Post a Comment